Jumanne , 4th Nov , 2014

Michuano ya Mpira wa Magongo ya Kumuenzi Baba wa Taifa inayofahamika kama Nyerere Cup inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba saba mpaka tisa mwaka huu mjini Moshi.

Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Timu ya Magereza ambao ni moja ya washiriki katika michuano hiyo, Merica Kahola amesema kikosi chake kinatarajiwa kuelekea Moshi Novemba Sita mwaka huu huku kikiwa na wachezaji18 pamoja na viongozi wanne ambapo wanatarajia kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Kahola amesema licha ya kuelekea katika michuano hiyo, timu inakabiliwa na changamoto mbalimbali hususani katika suala la vifaa ambapo ameiomba serikali kujitokeza kwa ajili ya kusaidia na kuendeleza mchezo huo hapa nchini.