Alhamisi , 26th Mar , 2015

Bondia Mohamed Matumla anatarajia kupanda ulingoni Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, hapo kesho kuzipiga na Bondia kutoka nchini China Wang Xin Hua katika pambano la uzito wa Super Bantam kuwania nafasi ya kugombea Ubingwa wa WBF.

Akiuzungumza jijini Dar es salaam, Rais wa Shirikisho la Ngumi nchini TPBO, Yassin Abdallah Ustaadh amesema, pambano hilo litatanguliwa na pambano la Japhet Kaseba na Mada Maugo, Thomas Mashali na Karama Nyilawila huku Ashraf Suleiman na Joseph Rabotte wa Marekani.

Ustaadh amesema, mabondia wanatakiwa kuheshimu kazi zao huku akiahidi kuimarisha ulinzi katika pambano hilo lenye ushindani mkubwa.