Jumanne , 8th Oct , 2019

Michuano ya Sprite Bball Kings iliyoandaliwa na East Africa TV na East Africa Radio kwa udhamini wa kinywaji cha Sprite imemalizika kwa Mchenga Bball Stars kuibuka mabingwa hii leo.

Mchezo wa tatu wa fainali ya Sprite Bball Kings 2019

Mchenga imeshinda ubingwa  baada ya kufanikiwa kushinda michezo mitatu ya fainali dhidi ya Tamaduni, ambapo katika mchezo wa tatu wa leo uliofanyika katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay, Mchenga imeshinda kwa vikapu 115 dhidi ya 109 vya Tamaduni, huku Baraka Sadick akifunga pointi 52, rebounds 3 na assists 3.

Ubingwa huo ni wa tatu mfululizo kwa Mchenga Bball Stars tangu mashindano yalipoanzishwa mwaka 2017, na mchezaji Baraka Sadick ameshinda tuzo ya MVP wa mashindano kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kushinda msimu uliopita akiwa na timu hiyo.

Bingwa wa michuano (Mchenga Bball Stars) imejinyakulia kitita cha Shilingi milioni 10 za Kitanzania, mshindi wa pili (Tamaduni) akijinyakulia kitita cha Shilingi milioni 3 huku MVP (Baraka Sadick) akijishindia Shilingi milioni 2.