Jumatatu , 8th Dec , 2014

Kocha wa Timu ya Mchezo wa Kriketi kutoka Nchini Kenya,Peter Ong'ondo amesema timu kutoka Tanzania na Uganda zimeendelea kuonyesha ubora katika michuano ya Afrika iliyoanza jana ambayo inaendelea Uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio,Ong'ondo amesema timu hizo zimeendelea kufanya vizuri japo katika kikosi chake anaona mabadiliko na anaamini atachukua ushindi katika michuano hiyo inayotarajiwa kumalizika hapo kesho.

Ong'ondo amesema mwaka jana walifungwa na Uganda pamoja na Tanzania lakini anaamini kikosi chake kimejiandaa kwa ajili ya kuchukua ushindi kutokana na mazoezi waliyoyafanya kwa takribani mwaka mzima.