Alhamisi , 20th Nov , 2014

Michuano ya Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi SHIMMUTA, imeanza leo Uwanja wa Mkwawani jijini Tanga kwa kushirikisha timu 21 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambazo zitashiriki michezo zaidi ya 10.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa SHIMMUTA, Award Safari amesema katika michuano hiyo inayotarajiwa kumalizika Novemba 30 mwaka huu ilitarajia kushirikisha timu zaidi ya 40 zilizoalikwa lakini zimeshindwa kutokana na michuano hiyo kukosa wadhamini ambapo amezitaka timu ambazo zinahitaji kushiriki kuhakiki ushiriki wao mpaka ifikapo kesho.

Safari amesema michuano hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba 22 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano,Samia Suluhu.