Alhamisi , 4th Dec , 2014

Mashindano ya mchezo wa Tenisi ya vijana yanatarajiwa kuanza Jumamosi ya wiki hii na kumalizika Jumapili jijini
Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Klabu wa mchezo huo, Hassan Kassim amesema mashindano hayo yatashirikisha vijana kuanzia umri wa miaka sita mpaka 18 na itashirikisha wavulana na wasichana.

Kassim amesema mashindano hayo yana lenga kutafuta timu itakayoshiriki michuano ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kufanyika January mwakani ambapo Tanzania itakuwa nchi mwenyeji.