Alhamisi , 13th Nov , 2014

Michuano ya wazi ya Tennis ya Klabu ya Kijitonyama ya jijini Dar es salaam inatarajia kufanyika Jumamosi ya wiki hii kwa kushirikisha wachezaji wa umri tofauti ikiwa na lengo la kupanga mipango ya kukuza mchezo huo katika klabu hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa klabu hiyo, Hassan kassim amesema michuano hiyo itasaidia kupata vipaji vipya na kukuza vipaji vilivyopo kwa vijana watakaoweza kushiriki mashindano mbalimbali.

Kassim amesema wanatarajia kujadili mashindano mbalimbali ya watoto ambao wamekuwa hawajiamini katika ushiriki wa mashindano ya wazi hivyo wanatarajia kuandaa mashindano.