Jumanne , 28th Oct , 2014

Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imesema imeamua kuitisha mkutano mkuu wa mwaka mapema zaidi tofauti na hapo awali ambapo ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa Klabu hiyo, Stephen Ally amesema mkutano huo utatoa nafasi kwa wanachama kutoa maoni mbalimbali juu ya kukuza na kuboresha klabu hiyo ambapo pia utajadili mambo mbalimbali ikiwemo suala la mwenendo mzima wa timu.

Ally amesema mpaka sasa hawajapanga tarehe rasmi kwa ajili ya mkutano huo na eneo utakapofanyika,lakini wanatarajia kukutana na viongozi wa Klabu hiyo mwishoni mwa juma hili kuweza kupanga tarehe rasmi na mahali utakapofanyika mkutano huo.