Jumapili , 30th Nov , 2014

Mkutano mkuu wa Kamati ya Olimpiki unatarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu Mkoani Morogoro kwa kushirikisha vyama mbalimbali vya michezo kutoka Tanzania Bara na visiwani.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi amesema lengo hasa la mkutano huo ni kuweza kujadili maendeleo mbalimbali ikiwemo rasimu ya bajeti kwa mwaka ujao ikiwa na lengo la maandalizi ya michuano mbalimbali.

Bayi amesema katika mkutano huo utasaidia kuweza kuzungumzia matatizo mbalimbali yaliyo ndani ya vyama vya michezo ikiwa na lengo la kukuza michezo nchini.