Jumanne , 1st Oct , 2019

Msemaji wa michuano ya Sprite Bball Kings 2019, Goza Chuma ameelezea maandalizi yanayoendelea kuelekea fainali ya michuano hiyo kati ya wababe Tamaduni na Mchenga Bball Stars.

Msemaji wa michuano ya Sprite Bball Kings 2019, Goza Chuma

Ikiwa ni siku tatu zimebaki kabla ya mchezo wa kwanza kupigwa katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay, Ijumaa hii ya Oktoba 4, Goza Chuma amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika, huku akiahidi kuwa 'surprise' mbalimbali zitakuwepo.

"Mpira wa kikapu hauna sare, ni lazima mshindi apatikane na ukija Ijumaa hii katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay, mshindi lazima apatikane kati ya Tamaduni na Mchenga. Lakini kutakuwa na wageni rasmi wazito tena sio mmoja ambao wameamua kuunga mkono kuwaangalia vijana", amesema Goza.

Fainali inatarajia kuwa na jumla ya michezo mitano, ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Ijumaa, Oktoba 4, mchezo wa pili Oktoba 6 na mchezo wa tatu ukitarajia kupigwa Oktoba 8.

Mtazame hapa chini akielezea zaidi.