Ni vita ya kisasi au heshima leo Yanga Vs Simba

Jumatano , 13th Jan , 2021

Fainali ya michuano ya Mapinduzi mwaka 2021 inapigwa leo usiku, uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar, ambapo miamba ya soka la Tanzania Simba na Yanga, itakuwa ikiumana kwenye mchezo huo wa fainali utakaopigwa Saa 2:15 Usiku.

Msimu huu kwenye mchezo wa ligi kuu Simba na Yanga zilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1

Yanga ndio walikuwa wa kwanza kutinga hatua ya fainali baada ya kuitoa kuitoa Azam FC kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Kwenye nusu fainali ya pili Simba SC waliitoa Namungo kwa kuifunga mabao 2-1 na Simba kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali ya pili mfululizo ya mashindano haya. Katika fainali ya msimu uliopita Simba SC walipoteza mchezo huo mbela ya Mtibwa Sugar.

Miamba hii miwili kutoka mitaa ya K/koo jijini Dar es salaam, itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kugawana alama kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2020-21 na mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.