Jumamosi , 2nd Jul , 2016

Mcheza tenisi namba moja kwa ubora duniani Novak Djokovic jioni ya jumamosi ya hii leo amejikuta akipata matokeo ya kushangaza baada ya kuondoshwa katika michuano mikubwa ya Grand Slam ya Wimbledon inayoendelea nchini Uingereza

Mcheza tenisi Sam Querrey aishangilia baada ya kumchapa Novak Djokovic.

Novak Djokovic ametolewa katika michuano ya tenisi ya Wimbledon baada ya kupata kipigo cha kustusha kutoka kwa raia wa Marekani Sam Querrey na kuzima kabisa ndoto na matumaini ya mchezaji huyo namba moja duniani kutwaa taji kubwa la michuano ya tenisi la Grand katika mwaka wa kalenda wa michuano ya tenisi.

Querrey, ambaye ni mchezaji namba 28 kwa ubora duniani alikamilisha ushindi wake katika raundi ya tatu ikiwa ni baada ya mvua kuahirisha mchezo jumamosi jioni.

Huo unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa raia huyo wa Serbia Novak Djokovic kupoteza katika michuano mikubwa ya major tangu alifanya hivyo katika fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa [French Open final] mnamo mwaka 2015.

Djokovic alikuwa na matumaini ya kushinda taji la tatu mfululizo la michuano hiyo ya Wimbledon na kuwa taji kubwa la tatu katika michuano ya msimu ya Grand Slam secure the third leg of a calendar Slam.

Djokovic mwenye miaka 29 alikuwa tayari ameshashinda mataji ya michuano mikubwa ya wazi ya Australia na Ufaransa mwaka huu na alikuwa pia akitka kujaribu kuwa mtu wa pili kushinda mataji makubwa matano.

Akizungumzia ushindi wake mchezaji Querrey mwenye miaka 28 amesema anajisikia ni mtu pekee sana na mwenye furaha isiyonakifani hasa baada yakufanikiwa kumsinda mchezaji bora wa tenisi duniani na kikubwa mchezaji ambaye amekuwa akitawala mashindano mbalimbali katika historia ya tenisi.