Jumamosi , 21st Sep , 2019

Michezo ya kwanza ya hatua ya nusu fainali ya Sprite Bball Kings 2019 imemalizika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa na kushuhudia mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars na Tamaduni wakianza vyema.

Michezo ya kwanza hatua ya nusu fainali, Sprite Bball Kings 2019

 

Michuano hiyo inayofanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo, ikiandaliwa na EATV na EA Radio kwa kushirikiana na kinywaji cha Sprite, imeonesha kuwa na msisimko mkubwa hasa katika hatua muhimu za kuelekea mwishoni.

Katika mchezo wa kwanza leo, timu ya Tamaduni imefanikiwa kuibuka na ushindi wa vikapu 99 dhidi ya vikapu 78 vya KG Dallas huku mchezaji Atupele Joseph wa KG Dallas akiongoza kwa kufunga pointi nyingi, ambapo amefunga jumla ya pointi 25, 'rebounds 5' - na 'assist 1'-.

Katika mchezo wa pili, mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars wameibuka na ushindi wa vikapu 95 dhidi ya 71 vya Flying Dribblers, huku mchezaji Baraka Sadick wa Mchenga akiongoza kwa kufunga pointi nyingi, ambapo amefunga pointi 35, 'rebounds 6' - na 'assist 3'.

Mechi za pili zinatarajia kupigwa Jumatano Ijayo, Septemba 25 katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.