Jumatano , 27th Oct , 2021

Mchezaji wa Zamani wa Chelsea na Arsenal, Oliver Giroud ameiongoza AC Milan katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Torino katika ligi kuu ya Italia, Seria A na kufikisha idadi ya alama 28 baada ya michezo kumi.

Wachezaji wa AC Milan wakishangilia ushindi

Giroud ambaye ni mshindi wa kombe Dunia 2018 akiwa na Ufaransa, ameweka rekodi ya kufunga mabao manne msimu huu ambapo magoli yote ameweka wavuni katika Dimba la San Siro.

Milan wanaongoza ligi kwa tofauti ya Alama tatu nyuma ya Napoli ambao watashuka uwanjani kucheza dhidi ya Bologna siku ya Alhamis ya Oktoba 28.

Mechi zingine zilizopigwa usiku wa jana ni Spezia walitoka sare ya bao 1-1 na Genoa, Venezia wakiwa nyumbani walikubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Salernitana.

Ratiba ya michezo ya Seria A leo, Oktoba 27 ni Sampdoria wataikalibisha Atalanta , Sassuolo watakuwa ugenini dhidi ya Juventus huku mechi ya mwisho ikiwa kati ya Mabingwa watetezi Internazionale Milan watasafiri kuifuata Empoli.