Real Madrid yapata pigo lingine kisa Covid-19

Jumanne , 6th Apr , 2021

Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, klabu ya Real Madrid itamkosa mlinizi wake wa kati tegemeo Rafael Varane kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza dhidi ya Liverpool saa 4:00 leo usiku baada ya nyota huyo kukutwa na maambukizi ya Covid-19 asubuhi ya leo.

Mlinzi wa Real Madrid, Rafael Varane mwenye maambukiz ya Covid-19.

Kukosekana kwa nyota huyo kunazidi kumpasua kichwa kocha wa klabu hiyo, Zinedine Zidane ambaye anawakosa walinzi wake tegemezi wa chaguo la kwanza baada ya Sergio Ramos kupata majeraha juma lililopita hivyo atalazimika kuwatumia walinzi Nacho Fernandez na Eder Militao.

Kwa upande mwingine,

Manchester City ya England pia itashuka dimbani saa 4:00 leo usiku tarehe 6 Aprili 2021 kukipiga na Borussia Dortmund ya Ujerumani kwenye mchezo mwingine wa robo fainali ya michuano hiyo utakaochezwa usiku wa leo kwenye dimba la Etihad, huku Dortmung ikitaraji kuwakosa nyota wake watatu ilhali Manchester City wakiwa fiti.

Wachezaji wa Dortmund watakaokosekana ni winga wake, Jadon Sancho mwenye maumivu ya misuli ya paja, mlinzi Dan-Alex Zagadou na kiungo Axel Witsel hivyo kuifanya timu hiyo kujivunia uwzo wa nyota wao Erling Haaland ambaye ni kinara wa ufungaji kwenye michuano hiyo akiwa na mabao 10.

(Winga tegemezi wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho).