Jumamosi , 14th Mei , 2022

Mchezo wa fainali ya kombe la FA (FA Cup) nchini England unaozikutanisha Livepool na Chelsea leo jioni, mchezo unaochezwa katika dimba la Wembley Jiji London England ni fainali ya 141 ya michuano hii mikongwa kabisa Duniani.

Chelsea na Liverpool zinakutana kwenye fainali ya FA Cup kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012

Liverpool hawajatwaa ubingwa wa michuano hii tangu mwaka 2006 takribani miaka 16 imepita, hivyo kocha Jurgen Klopp anakibarua cha kuhakikisha anawapa furaha mashabiki wa klabu hiyo kwa kushinda taji hili.

Hizi ni baadi ya rekodi za Liverpool na Chelsea kwenye michuano ya kombe la FA (FA Cup)

Hii ni fainali ya 16 ya michuano hii Chelsea wanacheza na wameshinda taji hili mara 8 katika fainali 15 walizocheza mpaka sasa mara ya mwisho wameshinda ubingwa wa michuano hii ilikuwa 2018. Liverpool fainali ya leo ni ya 15 wanacheza na ni mabingwa mara 7 mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa michuano hii ilikuwa 2006.

Chelsea wamecheza fainali 4 za FA Cup katika misimu 5 iliyopita lakini wameshinda kombe hili mara 1 tu katika fainali hizo. Na msimu uliopita walifungwa na Leicester City katika mchezo wa fainali.

Mara ya mwisho Chelsea na Liverpool kukutana kwenye fainali ya FA Cup ilikuwa mwaka 2021. The Blues Cheslea walishinda kwa mabao 2-1.