Alhamisi , 7th Jul , 2022

Mchezo wa ufunguzi wa michuano ya soka ya mataifa barani Ulaya ya wanawake katia ya timu ya taifa ya England na Austria umeweka rekodi ya kuhudhuriwa na watazamaji wengi katika historia ya michuano hiyo. Jumla ya mashabiki 68,871 wamehudhuria mchezo huu katika dimba la OLD Traford.

Mashabiki 68,871 wameutazama mchezo wa England na Austria katika dimba la Old Traford

Idadi hiyo ya watazamaji waliojitokeza katika Dimba la Old Traford ambao ni uwanja wa nyumbani wa Manchester United wamevunja rekodi ya idadi ya watazaji 41,301 walioshuhudia mchezo wa fainali ya Michuano ya Euro ya wanawake ya mwaka 2013 katia ya timu ya taifa ya Ujerumani na Norway uliochezwa katia dimaba la Friends Arena Stockholm Sweden, ambao ndio ulikuwa unashikiria rekodi ya kuhudhuriwa na watazaji wengi.

Kwa mujibu wa ripoti jumla ya tiketi 517,000 zimeuzwa kati ya tiketi 700,000 za michuano hii. Katika aridhi ya Uingereza bado rekodi ya watazamaji 80,203 walijitokeza kushuhudia mchezo wa fainali ya wanawake ya michuano ya Olimpiki mwaka 2012 kati ya timu ya taifa ya Marekani na Japan uliochezwa uwanja wa Wembley ndio mchezo ulioshuhudiwa na watazamaji wengi zaidi.

Na katika mchezo huu wenyeji wa michuano hii timu ya taifa ya England imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Austria kwenye mchezo wa kundi A. Bao la pekee kwenye mchezo huu limefungwa na Beth Mead dakika ya 16. Michuano hii inaendelea tena leo kwa mchezo mmoja wa kundi A ambapo Norway wataminyana na Ireland ya Kaskazini majira ya Saa 4 Usiku.