Jumatano , 19th Nov , 2014

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Kriketi, Khalil Remtullah amesema anaamini timu yake itafanya vizuri katika michuano ya wasichana ya kuwania kushiriki michuano ya kombe la Dunia itakayofanyika Desemba 12 mpaka 17 Afrika Kusini

Akizungumza na East Africa Radio, Ramtullah amesema wachezaji wote wapo kambini na wanaendelea na mazoezi ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na michuano hiyo.

Remtullah amesema kuwa awali alianza kwa kuwapa wachezaji wake mazoezi ya kawaida lakini hivi sasa anaendelea na mazoezi ambayo yatawajenga kwa ajili ya michuano hiyo yenye ushindani mkubwa.