Jumapili , 8th Sep , 2019

Hatua ya 16 bora ya michuano ya Sprite Bball Kings 2019 imekamilika leo katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Matukio ya siku ya pili ya hatua ya 16 bora

Katika hatua hiyo, jumla ya timu nane zimefuzu hatua ya robo fainali ambapo nne za kwanza zilifuzu jana Jumamosi na zingine nne kufuzu hii leo.

Mchezo wa kwanza hii leo, umeshuhudiwa Ukonga Hitmen ikiibuka na ushindi wa vikapu 107 dhidi ya 74 vya JK Ballers huku katika mchezo wa pili, K.G Dallas imeshinda kwa vikapu 79 dhidi ya 76 vya Wagalatia.

Katika mchezo wa tatu, TMT ( The Money Team ) imeibuka na ushindi wa vikapu 120 dhidi ya 84 vya Weusi na matokeo ya mchezo wa mwisho, Flying Dribblers nayo imetinga robo fainali kwa jumla ya vikapu76 dhidi ya 64 vya Oysterbay.

Droo ya robo fainali itafanyika kesho Jumatatu, Septemba 10 katika ofisi za EATV na EA Radio, Mikocheni Jijini Dar es Salaam saa 6 mchana.