Alhamisi , 26th Mei , 2016

Wakati Jose Mourinho akitarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Machester United, Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Cristiano Ronaldo ana imani na kocha huyo kurudisha hadhi ya Mashetani Wekundu hao.

Ronaldo aliyechezea United kwa misimu 6, amesema anaumia moyo kuiona klabu yake ya zamani ikiwa katika hali mbaya, na ujio wa Mourinho utaisaidia klabu hiyo kurudisha makali yake.

Aidha, Mreno huyo amekataa kuongelea bifu lake la zamani na Mreno mwenzake alipokuwa Kocha wa Real Madrid, na kusema hayo yameshapita.