Jumatatu , 18th Mei , 2015

Shule za sekondari zilizoko mkoani Morogoro zimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati FEASSA yatakayofanyika mwaka huu nchini Rwanda.

Akizungumza na East Africa Radio, mmoja wa walimu wa michezo katika shule za mkoani hapo, Mohamed Majaliwa amesema, vijana wameanza mazoezi yanayofanyika mara mbili kwa siku ambayo anaamini yatawasaidia kujiweka vizuri katika maandalizi ya michuano hiyo.

Majaliwa amesema, wameamua kuanza mapema mazoezi ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuchukua ubingwa katika msimu huu.

Mashindano hayo mwaka jana yalifanyika jijini Dar es salaam, kwa kushirikisha shule mbalimbali za Sekondari kutoka nchini Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.