Alhamisi , 4th Jun , 2015

Semina kwa mabondia iliyoandaliwa na Shirikisho la Masumbwi nchini PST kwa kushirikiana na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBO inatarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es salaam kwa kushirikisha mabondia wanaotarajiwa kupambana Jumamosi.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa Chama cha Ngumi za kulipwa Antony Rutta amesema pambano hilo litakalofanyika Uwanja wa ndani wa Taifa litakuwa ni lakuwania ubingwa wa Dunia kwa kuwakutanisha Mabondia Allan Kamote na Bondia kutoka Kenya Emilio Novat.

Rutta amesema, pambano hilo litatanguliwa na mapambano manne ya utangulizi ambapo James Onyango na Ramadhan Shauri wakipambana kuwania mkanda wa kimataifa, Dulla Mbabe na Omary Tamba, Thomas Mashali na Suleiman Tall huku Cosmas Cheka akipambana na Saidy Mundi.