Ijumaa , 12th Dec , 2014

Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA,imeitaka serikali na watu binafsi kujitokeza kusaidia mchezo huo hapa nchini ili kuweza kushiriki na kukuza vipaji vya vijana.

Akizungumzas na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa DAREVA, Yusuph Mkarambati amesema vilabu vingi vinashindwa kushiriki mashindano mbalimbali hususani yanayoendelea hivi sasa ya Kombe la Uhuru ambapo timu Tano za wanaume na Mbili za wanawake kutoka mkoa wa Dar es salaam ndizo zilizojitokeza kushiriki.

Mkarambati amesema licha ya timu nyingi kushiriki katika mashindano mengine yanayoendelea lakini kikubwa kinachofanya vilabu vingine kushindwa kushiriki ni kutokana na kukosekana kwa wadhamini ili kusaidia mchezo huo kukua zaidi hapa nchini.