Alhamisi , 29th Mei , 2014

Serikali imesema jezi za sasa za timu ya taifa ya Tanzania taifa stars ni ruhksa kwa TFF kuzifanyia mabadiliko kutokana na wadau wengi kulalamikia kuwa haziendani na rangi ya bendera ya taifa

Kikosi cha timu ya taifa stars kikiwa na jezi mpya ambazo zitabadilishwa.

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya habari , vijana, utamaduni na michezo imesema itaiagiza mara moja shirikisho la soka nchini TFF kuachana na mpango wa kubadilisha jina la timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars.

Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia amesema hayo wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha bunge la bajeti kinachoendelea mkoani Dodoma huku akianzia na suala la kubadilishwa kwa jezi za timu hiyo ambazo zinatumika hivi sasa.

Mh. Nkamia amesema awali walipata taarifa kutoka TFF kuhusiana na jezi ambazo taifa stars inazitumia hivi sasa wakidai jezi za awali ambazo rangi yake ya Blue iliyokolea ilikua ikisababisha mgongano wa rangi wakati wa kupiga picha hasa kupitia luninga na hivyo Wizara yake imewapa ruhusa TFF kuendelea na mchakato wa upatikanaji wa jezi bora za taifa stars zitakazoendana na rangi ya bendera ya taifa na pia rangi ambayo haitakuwa kikwazo katika picha za luninga.