Jumanne , 29th Apr , 2014

Serikali ya Tanzania imezitaka timu zinazokwenda kushiriki katika michuano ya Jumuiya ya Madola kuhakikisha zinarejea na medali ili kuiletea sifa Taifa

Baadhi ya wachezaji na viomgozi wa michezo wanaokwenda kushiriki michuano ya madola, wakikabidhiwa bendera

Serikali ya Tanzania imezitaka timu zinazokwenda kushiriki katika michuano ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika mwezi July mwaka huu jijini Glascow nchini Scotland kuhakikisha zinarejea na medali ili kuiletea sifa Taifa na kutoziangusha nchi wanazokwenda katika mfunzo ya maandalizi ya michuano hiyo.

Akizungumza hii leo jijini Dar es salaam wakati akiziaga na kuzikabidhi Bendera ya Taifa timu tano za michezo ya Riadha, Ngumi Judo, Kuogelea na Mpira wa Meza, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema kushinda katika michuano hiyo kutazifurahisha nchi zilizoshiriki katika maandalizi.

Kwa upande wake, Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania TOC, Filbert Bayi amewataka wachezaji wataokwenda katika mafunzo hayo muhimu kufuata kilichowapeleka na kuzingatia mafunzo ili kufanikiwa katika michuano ya Jumuiya ya Madola.

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho wa Riadha Tanzania RT, Antony Mtaka akiongea kwa niaba ya Viongozi wa Vyama vyenye wachezaji wanaokwenda katika mafunzo hayo amewataka kuhakikisha wanashinda katika michuano hiyo ili kufungua fursa kwa wadhamini

Nahodha wa timu ya Mpira wa Meza Agnes Ngodoki pamoja na Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania BFT, Mutta Rwakatare wameishukuru serikali kwa kupata nafasi hiyo na kuahidi kurejea na Medali