Jumatatu , 1st Dec , 2014

Serikali imetakiwa kuondoa kodi ya vifaa vya michezo hususani katika mchezo wa mpira wa magongo ili kuwa na urahisi wa kununua vifaa hivi.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania THA, Abraham Sykes amesema wameanza programu ya kutoa mafunzo ya mchezo huo kwa shule mbalimbali nchini, lakini vifaa vimekuwa vichache suala linalochangia elimu ya mchezo huu kushindwa kuwafikia wanafunzi wengi nchini.

Sykes amesema wazazi pia wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kusaidia mchezo huu hususani ka upande wa kununua vifaa vya mchezo huo kwa wanafunzi ili kuweza kuukuza mchezo huu hapa nchini.