Ijumaa , 9th Aug , 2019

East Africa Television na East Africa Radio ikipewa nguvu na kinywaji cha Sprite, imeandaa mashindano ya mpira wa kikapu kwa wanaume ya Sprite Bball Kings yanayotarajia kuanza hivi karibuni kwa msimu wa tatu.

Mshindi wa Sprite Bball Kings 2018

Ufunguzi wa michuano hiyo utafanyika Agosti 17 Mlimani City kuanzia saa 3:00 asubuhi, ambapo matukio kadhaa yatafanyika ikiwemo usajili wa timu shiriki za michuano hiyo.

Matukio mengine yatakayofanyika ni 'Rap Battles', kufanya mitupio ya nguvu 'ku dunk', three pointers, kucheza na vitu vingine vingi.

Baada ya michezo hiyo, kitafuatiwa chakula cha mchana pamoja na mastaa mbalimbali ambao wamealikwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano.

Mashindano ya mwaka huu yanafanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo. Timu zote zinazokidhi vigezo zinaalikwa kushiriki katika michuano hiyo ili kuleta ushindani mkubwa zaidi.

Endelea kufuatilia EATV na EA Radio pamoja na EATV&Radio Digital kupata taarifa zaidi kuhusu michuano hii.