Jumatano , 20th Mei , 2015

Stand United imetamba kuwa msimu ujao hautakuwa wa kugombea kuteremka daraja kama ilivyokuwa msimu huu.

Mkurugenzi wa ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu amesema wana kila sababu ya kufanya vizuri kwa kuwa wanajua wapi wanatakiwa kufanya marekebisho.

Kanu amesema, msimu ujao hauwezi kuwa kama uliomalizika na wanatengeneza kikosi bora ambacho sasa kitakuwa ni cha kuwania ubingwa na si vinginevyo.

Stand imefanikiwa kuondoka katika janga hilo katika hatua ya mwisho baada ya kuitwanga Ruvu Shooting kwa bao 1-0 katika mechi yake ya mwisho ya ligi kuu Bara kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.