Jumatano , 20th Mei , 2015

Baada ya kuanza kwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Swaziland katiika michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini, Timu ya Soka ya Tanzania Taifa Stars leo tena inatupa karata yake ya pili dhidi ya Madagascar.

Stars watatakiwa kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga katika hatua ya robo fainali.

Stars wanakutana na Madagascar ambayo mchezo wake wa kwanza ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Lesotho ambao wapo kundi moja kila timu ikihitaji ushindi kwa namna yoyote ile.

Stars wakimaliza mchezo huo watakuwa na kibarua kingine Ijumaa dhidi ya Lesotho michezo yote hiyo ikichezwa katika uwanja wa Moruleng ambapo ndipo itajulikana kama timu hiyo itasonga mbele au itayaaga mashindano hayo.