Jumatano , 27th Oct , 2021

Uhondo wa Ligi Kuu Tanzania bara unarejea tena leo kwa michezo miwili kuchezwa katika viwanja viwili tofauti, uwanja wa Nelson Mandela mjini sumbawanga mkoani Rukwa itashuhudia Prizons wakiwakaribisha Biashara united kutokea Musoma mkoani Mara ilhali Simba baada ya kujeruhiwa na Jwaneng ga

Kiungo Mzamiru Yassin akijaribu kukatiza kati kati ya msitu wa wachezaji wa Polisi Tanzania katika mchezo wa msimu uliopita.

Mpaka sasa magoli 37 yamefungwa katika michezo 54 sawa na wastani wa goli 1.45 kwa kila mchezo huku vilabu vya Polisi Tanzania,Yanga na Mbeya Kwanza zikiwa zimecheza michezo mitatu na hawajaonja ladha ya kipigo kama ilivyo kwa Simba waliocheza michezo miwili na mbeya city aliyecheza michezo minne bila kupoteza mchezo mpaka sasa.

Rekodi tamu kwa mashabiki wa Yanga ni kuishuhudia timu yao ikicheza dakika 270 huku Simba wakicheza dakika 180 wakiwa ndio timu pekee ambazo hazijaruhusu goli lao kufungwa mpaka sasa.

Polisi Tanzania ndio Klabu kinara wa Ligi na magoli ambapo katika michezo mitatu wakifunga magoli 5 huku mshambuliaji Vitalis Mayanga mwenye magoli 3 akiongoza mbio za ufungaji bora hadi sasa.

Timu ya Geita gold ndio timu iliyoruhusu magoli mengi ambayo ni matano wakati Biashara United ndio klabu yenye safu butu ya ushambuliaji wakicheza dakika 180 bila ya kufunga goli hata mmoja wakati Mbeya City anaongoza kwa kupata sare katika michezo mitatu kati ya minne waliyoicheza

Mchezo katika uwanja wa Nelson Mandela baina ya Tanzania Prisons dhidi ya Biashara utakuwa ni vita ya kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi baina ya anayeburuta mkia kwenye msimamo akiwa na alama 1 kwenye michezo 3 iliyocheza klabu ya Tanzania prisons dhidi ya Biashara United ya mara yenye alama moja na yenyewe mpaka sasa ikikamata nafasi ya 15 .

Mbeya derby baina ya Mbeya city dhidi ya Mbeya Kwanza ikatuandikishia rekodi ya mchezo ulioweka ''comeback'' ya hatari mpaka sasa,mbeya city wakiongoza kwa magoli 2 kwa 0 lakini dakika 10 zilimtosha mshambuliaji Crispin Ngushi kufunga magoli mawili dakika 78 , 88 kulazimisha sare kwenye derby hiyo.

Kati ya timu 16, makocha wa kigeni wakiwa ni 10 na wazawa ni sita tu ilhali makocha wawili washapewa mkono wa kwaheri wa kwanza akiwa mburundi Etiene Ndairagije aliyeiongoza Geita gold katika michezo minne na kufungwa michezo 2 na sare michezo 2 sasa kibarua chake kitashikwa kwa muda na fred felix minziro.

Mfaransa Didier Gomez da Rossa baada ya mafanikio ya kuifikisha simba hatua ya robo fainali na kuwapa makombe mawili ya ubingwa wa ligi kuu na kombe la Fa kibarua chake kimeota nyasi baada ya kuwaongoza lunyasi katika michezo miwili pekee,akishinda mmoja na kupata sare mchezo mmoja ndani ya msimu huu na sasa kibarua chake kitashikwa kwa muda na Thierry Hitimana.