Jumatano , 25th Sep , 2019

Nusu fainali ya Sprite Bball Kings 2019 imekamilika usiku wa leo katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay ambapo nusu fainali za pili kati ya 'Best of three' zimepigwa.

Matukio ya nusu fainali ya pili ya Sprite Bball Kings 2019

Katika mchezo wa kwanza leo, Tamaduni imeibuka na ushindi wa vikapu 116 dhidi ya 65 vya KG Dallas huku mchezaji, Cornel Joseph wa Tamaduni akifunga pointi 28, rebounds 10 na assist 1. Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wiliendi iliyopita, Tamaduni iliibuka na ushindi wa vikapu 99 dhidi ya 78 vya KG Dallas.

Mchezo wa pili wa leo, Mchenga Bball Stars imeibuka na ushindi wa vikapu 105 dhidi ya 72 vya Flying Dribblers huku mchezaji, Baraka Sadick wa Mchenga akifunga jumla ya pointi 49, rebounds 2 na assist 2. Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wiliendi iliyopita, Mchenga Bball Stars iliibuka na ushindi wa vikapu 95 dhidi ya 71 vya Flying Dribblers.

Kwa ushindi huo wa leo, ni rasmi kuwa fainali ya Sprite Bball Kings 2019 itakuwa kati ya Tamaduni na Mchenga Bball Stars baada ya kufanikiwa kushinda nusu fainali mbili kati ya tatu dhidi ya wapinzani wao.