Jumanne , 22nd Jul , 2014

Chama cha mchezo wa Rollball Tanzania TRBA kimepata baraka za kuwa mwenyeji wa michuano ya Rollball Afrika kwa mara ya kwanza kutoka chama cha Rollball Afrika, ambapo kwa sasa TRBA wanaangaikia udhamini ili kufanikisha michuano hiyo

Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya rollball ya Tanzania wakijifua.

Tanzania inataraji kuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza wa michuano ya Afrika mchezo wa Rollball mashindano yatakayoanza August 26 hadi 30 mwaka huu yakifanyika katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam

Rais wa chama cha mchezo wa rollball Tanzania TRBA Noel Kihunsi amesema maandalizi ya michuano hiyo yanakwenda vizuri na wamepata Baraka zote kutoka serikalini kupitia baraza la michezo nchini BMT

Kihunsi amesema wanataraji timu nyingi kushiriki michuano hiyo na mpaka sasa ni nchi za Uganda, Kenya na Rwanda ndizo zimethibitisha kushiriki michuano hiyo mpaka sasa

Aidha Kihunsi amesema kufanyika michuano hiyo hapa nchini kwa mara ya kwanza itatoa fursa kwa Watanzania kuona mchezo huo kwani kwa miaka kadhaa Tanzania imekua ikishiriki michuano ambayo inafanyika nje ya nchi.