Jumapili , 15th Jun , 2014

Ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa na kuwa mwenyeji wa michuano ya mchezo wa Rollball barani Africa tangu mchezo huo umeanza kuenea kwa mara brani Africa

Wachezaji wa mchezo wa Rollball wakichuana katika moja ya mashindano ya mchezo huo.

Tanzania inataraji kuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza kwa michuano mikubwa ya mchezo wa Rollyball kwa nchi za africa mashariki na kati itakayofanyika jijini Dar es salaam

Rais wa chama cha Rollball Tanzania TRBA Noel Kihunsi amesema baada ya kuwa na mpango wa muda mrefu wa kukuza mchezo huo hapa nchini hatimaye wamepata kibali cha kuandaa michuano hiyo kutoka shirikisho la Rollball barani africa na sasa baada ya kupata baraka zote toka kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wanataraji michuano hiyo ambayo itakua ikifanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ianze rasmi August 28 hadi 31 mwaka huu

Aidha Kihunsi amesema kila kitu katika maandalizi kiko sawasawa na tayari wao kama chama mwenyeji kimeshapeleka barua za mialiko kwa timu zote shiriki,

Kwaupande wake nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Rollball Tanzania Khosa Athuman amesema kikosi chao kiko tayari kwa michuano hiyo mikubwa na amewataka wadau kuisaidia timu hiyo hasa vifaa vya mazoezi ili waweze kujiandaa vema na michuano hiyo ili walibakize kombe hilo hapa nchini kwa mara ya kwanza.