Alhamisi , 13th Nov , 2014

Timu za Tanzania zimeendelea kufanya vizuri katika michuano ya wavu ya Kombe la Nyerere inayoendelea Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya Chama cha Mpira wa Wavu nchini TAVA, Somo Kimwaga amesema michuano ya mwaka huu imekuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka iliyopita ambapo ilizoeleka timu alikwa kutoka nchini Kenya zilizoeleka kufanya vizuri lakini kwa mwaka huu timu hizo zimeanza kwa kufungwa na timu kutoka Tanzania.

Kimwaga amesema kiwango cha timu za Tanzania kimepanda kutokana na kila timu kujiandaa ikijua itakutana na timu zilizojiandaa vilivyo katika michuano hiyo hivyo imesaidia kwa timu za Tanzania kuweza kufanya vizuri tofauti na miaka iliyopita.