Jumatatu , 1st Dec , 2014

Shirikisho la Soka nchini TFF,limesema mwakani linatarajia kuwa na makocha na waamuzi wanawake kutoka kila mkoa ili kuendelea kukuza soka kwa wanawake hapa nchini.

Akizungumza na East africa Radio, Mkurugenzi wa ufundi wa TFF, Salum Madadi amesema wanatarajia kutengeneza kozi maalumu ambapo kutakuwa na darasa lenye watu 35 ili kuweza kupata viongozi wa kutosha watakaoweza kusaidia kufanya mpira uweze kuchezwa.

Madadi amesema viongozi hao wataweza kusaidia kuweza kutoa elimu kwa mikoa mbalimbali nchini na kuwezesha kupata timu zitakazoweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.