Jumatano , 21st Mei , 2014

Shirikisho la soka hapa nchini TFF limepanga kuendesha semina maalumu kwa waandishi wa habari za mpira wa miguu ili kuwakumbusha namna sahihi ya kuripoti mchezo huo.

Boniface Wambura-afisa habari TFF

Shirikisho la soka hapa nchini TFF limepanga kuendesha semina maalumu kwa waandishi wa habari za mpira wa miguu ili kuwakumbusha namna sahihi ya kuripoti mchezo huo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na EATV, afisa habari wa shirikisho hilo bwana Boniface Wambura amesema kwamba watashirikiana na bodi ya ligi na wadhamini mbali mbali wa mashindano yaliyo chini ya shirikisho hilo ili kufanikisha mpango huo.

Aidha bwana Wambura amesema huu ni utaratibu wao wa siku nyingi na mara ya mwisho kufanya semina kama hiyo ilikuwa muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu uliopita wa TFF.