Ijumaa , 5th Jun , 2015

Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Jamal Malinzi amesema bado wanaendelea kutafakari suala zima la kujiuzulu kwa Rais wa Shirikisho la Soka ulimwenguni FIFA Sepp Blatter.

Akizungumza na East Africa Radio, Malinzi amesema, kuhusu suala zima la miradi iliyokuwa ikiendelea kutolewa na shirikisho hilo litaendelea kwa kuwa FIFA ni taasisi.

Blatter, raia wa Uswisi, ameamua kuachia ngazi baada ya kuwa kwenye usukani kwa miaka 17, tena akiwa ameshinda mara nyingine, lakini kashfa ya rushwa imemuondoa.