Jumatano , 14th Jan , 2015

SHIRIKISHO la soka nchini TFF limeizuia timu ya Polisi Mara kutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na matukio ya vurugu na uvunjifu wa amani ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za FDL zinazochezwa kwenye uwanja huo, ikiwemo ile ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga ambapo waamuzi walipigwa.

Kamati zinazohusika zitakutakana hivi karibuni kupitia matukio yote ya utovu wa nidhamu kwenye FDL, na hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ikiwemo na viwanja ambavyo vimekuwa na sifa ya vurugu.

Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vina wajibu wa kutoa ulinzi wa kutosha viwanjani wakati wa mechi.