Jumatano , 2nd Sep , 2015

Bodi ya ligi nchini TPLB imesema imeboresha ligi nchini kwa kuwa na waamuzi bora na wenye uwezo ili kuweza kupunguza upangaji wa matokeo katika michuano ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Afisa Mtendaji wa TPLB Boniface Wambura amesema, wameamua kufanyia kazi sehemu ya waamuzi ambayo msimu uliopita kulikuwa na malalamiko kutoka kwa vilabu wakiwalalamikia waamuzi kushindwa kuchezesha mchezo kwa haki.

Wambura amesema, wamechukua waamuzi wenye ngazi ya shirikisho la soka ulimwenguni FIFA ambapo mpaka sasa wapo tayari kwa ajili ya kuanza michuano ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu katika viwanja mbalimbali hapa nchini.