Jumanne , 20th Mei , 2014

Chama cha mchezo wa mpira wa meza Tanzania TTTA kuwaandalia mchezo wa kimataifa wakujipima nguvu wachezaji walioko katika kambi ya mazoezi ya maandalizi ya madola pindi watakaporejea kutoka nchini China.

Chama cha mpira wa meza Tanzania TTTA kimesema pamoja na baadhi ya wachezaji wake kwenda nchini china kujiandaa na michuano ya madola wao kinaendelea na program zake kama kawaida.

Chama hicho pia kinaendelea kumuandaa mchezaji mmoja aliyebaki nchini ambaye baadaye ataungana na wenzake watano walioko china kwa kambi ya miezi miwili wakijiandaa na michuano ya madola itakayofanyika jijini Grascow Scotland Julai mwaka huu.

Katibu mkuu wa TTTA Issa Mtalaso amesema wanaendelea na maandalizi ya michuano hiyo na wanaipongeza serikali kwa kuwapa fursa wanamichezo wakajiandae nje ya nchi kwakuwa fursa hiyo itawasaidia kuongeza uwezo na mbinu kwa ujumla na baadaye kuwawezesha wachezaji hao kufanya vema katika michuano mbalimbali iliyo mbele yao wakianzia na hii ya Jumuiya ya Madola.