Jumapili , 25th Sep , 2022

Promota wa bondia Anthony Joshua, Eddie Hearn amesema hawatasaini mkataba wa makubaliano ya Pambano la mabondia waingereza Joshua na Tyson Fury haraka kama Fury anavyotaka.

Bondia Anthony Joshua kushoto, na Tyson Fury upande wa kulia

Hearn amemjibu Tyson Fury ambaye ni bingwa wa uzito wa juu wa mkanda wa WBC baada ya bondia huyo kusema anataka kambi ya Joshua kusaini mataba wa makubaliano ya pambano lao linalotarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu kesho Jumatatu.

‘’Nadhani hakuna njia yoyote mkataba huu utasainiwa Jumatatu kwa sababu bado kuna mengi ya kufanywa. Pambano hili litachukua muda. Tulisubiri siku 10 kupata mkataba ghafla anataka usainiwe ndani ya masaa 24. Haiwezekani.’’ Amesema Eddie Hearn

Hearn ameenda mbali na kusema kuwa Fury anataka kuepuka pambanao lake dhidi ya Joshua ndio maana anaweka masharti, na ameweka wazi kuwa Tyson Fury anataka kupigana na bondia Mjerumani Mahmoud Charr.