Jumanne , 24th Jan , 2023

Beki wa mpya wa klabu ya Yanga Mamadou Doumbia amewaambia mashabiki wa Yanga kuwa yeye sio mtu wa maneno sana bali ataacha vitendo vyake vizungumze uwanjani

Doumbia amesajiliwa na Yanga akitokea katika timu ya Stade Malien ya nchini Mali kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.

“Nimefurahi sana kufika hapa, Yanga ni klabu kubwa sana kule Mali, inafatiliwa na watu wengi hivyo kuja hapa ni jambo kubwa sana kwangu kama mchezaji.

“Mimi sio mtu wa maneno sana, kazi yangu ni uwanjani na mashabiki wategemee mazuri kutoka kwangu, nawapenda sana,” alisema Doumbia

 

Yanga imeendeleza rekodi yake ya kufunga bao kwenye kila mechi ya ligi kwa msimu huu, ikifikisha mabao 39.

Ushindi huo  wa jana dhidi ya Ruvu Shooting umewafanya Wanajangwani, Yanga kufikisha alama 53 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi, pointi sita zaidi ya Simba inayofuata ikiwa nazo 47 nafasi ya pili.