Jumanne , 4th Nov , 2014

Wamiliki wa viwanja ambavyo vitatumika katika michuano ya Ligi Daraja la pili SDL inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu katika viwanja mbalimbali nchini wametakiwa kufanyia marekebisho viwanja hivyo kabla ya kuanza kwa Ligi hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka nchini, Boniface Wambura amesema kuna baadhi ya viwanja ambavyo havikuwa katika hadhi ya kuchezwa Ligi hiyo hadi vifanyiwe marekebisho na kuna baadhi ya viwanja vinatakiwa marekebisho madogomadogo ambayo yanarekebishika hivyo wajitahidi kumaliza marekebisho hayo ili Ligi ianze kwa wakati uliopangwa.

Wambura amesema kama kuna timu ambayo inakuwa haijakamilisha ukarabati wa uwanja utakao tumika,itawalazimu kutafuta uwanja ambao utafaa kwa ajili ya kutumia katika mechi mbalimbali za Ligi hiyo.