Jumatatu , 23rd Feb , 2015

Michuano ya Mpira wa wavu Klabu Bingwa Mkoa wa Dar es aalaam yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Shule ya Uhuru jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Siraju Mwasha amesema, mashindano hayo yenye lengo la kukuza mchezo huo yatashirikisha vilabu mbalimbali vya jiji la Dar es salaam ambavyo vitakuwa vimekwishahakiki ushiriki wa michuano hiyo.

Mwasha amesema, vilabu mbalimbali vimeanza uhakiki wa ushiriki wake ambapo michuano hiyo itakuwa ikifanyika Jumamosi na Jumapili huku kukiwa na sehemu mbili huku ya kwanza itamalizika Aprili huku ya pili ambayo ni yakujua mshindi itamalizika Agosti mwaka huu.

Mwasha amesema, michuano hiyo itasaidia kuendeleza vipaji vya washiriki wa michuano hiyo kutokana na michuano hiyo kufanyika mara kwa mara na kwa muda mrefu ambapo itasaidia wanamichezo hao kuwa na uwezo na nguvu ya kuendelea kushiriki mashindano hayo.