Alhamisi , 27th Nov , 2014

Vyama vya mikoa vya mpira wa kikapu nchini vimetakiwa kuchagua timu yenye uwezo wa kufanya vizuri katika michuano ya kitaifa ili kuweza kupata timu ya Taifa itakayoweza kuliwakilisha taifa katika mashindano mbalimbali.

Akizungumza na East Africa Radio, Manase Zabroni amesema katika michuano ya Kitaifa inayoendelea Mkoani Dodoma, mikoa iliyokuwa ikishiriki michuano hiyo kila mwaka tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo imeonekana ikifanya vizuri zaidi kutokana na maandalizi pamoja na ushiriki wa mara kwa mara.

Zabroni amesema vilabu vinatakiwa kufanya maandalizi ya mapema ikiwa ni pamoja na kushiriki mashindano ya mara kwa mara ili kujihakikishia kufanya vizuri katika michuano mbalimbali mikubwa hapa nchini na nje ya nchi.