Ijumaa , 15th Mei , 2015

Waamuzi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za mchezo huo ili kuweza kuendana na kasi ya mchezo katika ligi ya taifa ya kikapu inayoendelea uwanja wa ndani wa taifa, jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, mmoja wa makocha wanaosimamia michuano hiyo, Bahati Mgunda amesema, ligi hiyo imekuwa na changamoto nyingi na kiwango cha waamuzi haujafikia katika hatua inayotakiwa.

Mgunda amesema katika ligi hiyo ni kunatakiwa waamuzi watatu lakini mpaka sasa wana waamuzi wawili lakini anaamini malengo ya kukuza mchezo huo yatafanikiwa na pia waamuzi watafikia ile hatua inayohitajika.