Ijumaa , 17th Oct , 2014

Waamuzi wa soka nchini wametakiwa kuwa makini katika mechi mbalimbali hapa nchini hususani za Ligi Daraja la kwanza ili kuweza kupata vijana wenye vipaji watakaoweza kuliwakilisha taifa katika mechi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Waamuzi

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Timu ya Lipuli FC, Haruna Salehe amesema iwapo waamuzi hao watatenda haki katika mechi hizo, watapata timu nzuri na zenye wachezaji wazuri.

Salehe amesema iwapo waamuzi hao watazingatia sheria na kanuni zilizopo katika soka, nchi itaweza kupata wachezaji wazuri na wenye vipaji.