Jumatatu , 17th Nov , 2014

Timu ya wanawake ya mpira wa magongo ya Tanzania inatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea nchini Zimbambwe kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika inayotarajiwa kuanza Novemba 22 mpaka 30 nchini humo.

Akizungumza na East Africa Radio,Katibu wa Chama cha mpira wa Magongo Mkoani Dar es salaam DRHA,mnonda Magani amesema michuano hiyo inashirikisha nchi 10 ambapo timu inatarajia kuondoka na wachezaji 15 pamoja na viongozi wawili.

Magani amesema,hivi sasa wapo katika mchakato wa kuhakikisha wanakuza vipaji vya wachezaji hususani wanawake katika mchezo huo ili kuwawezesha kuweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.