Ijumaa , 8th Apr , 2016

Pamoja na kamati ya nidhamu ya TFF kutoa adhabu kwa wale waliohusika katika kesi ya upangaji wa matokeo ya michezo ya mwisho ya ligi daraja la kwanza kundi C, Clip ya sauti za vigogo wa TFF iliyosambaa mitandaoni yatoa sura mpya ya kesi hiyo.

Rias wa TFF Jamal Malinzi akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawako pichani katika moja ya mikutano yake.

Sakata la tuhuma za rushwa na upangaji matokeo katika michezo miwili ya mwisho la ligi daraja la kwanza Tanzania bara FDL kundi C limechukuwa sura mpya baada ya kusambaa kwa clip ya sauti zinazosemekana ni za viongozi wa juu na maofisa wa shirikisho la soka nchini TFF.

Kusambaa kwa clip hiyo ambayo wadau wa soka nchini wanafamilia ya mpira wengi wao wamekiri na kuthibitisha kuzifahamu sauti za wahusika hao wamesema kama hali iko hivyo basi arobaini ya wabadhilifu katika mchezo wa soka waliochangia kushusha soka nchini kwa muda mrefu imetimia na sasa ni wazi imefichuka kuwa mpira wetu ulikuwa ukiendeshwa kwa magumashi na mazingira ya wazi ya rushwa na ubadhilifu uliopindukia huku watu wakitumia mpira kujinufaisha wao binafsi na kuwaacha wapenzi wa soka wakiumia kwa matokeo hayo waliyoyasababisha wao kwa makusudi.

Wakizungumzia kashfa hiyo ama sakata hilo ambalo limeteka vichwa vya habari hapa nchini na kuchukua nafasi kubwa katika mitandao ya kijamii baadhi ya wadau wa soka nchini wameonyesha kuchukizwa na kusikitishwa sana na sakata hilo na kudiliki kumtaka wazi wazi rais wa TFF Jamal Malinzi kuwajibika kutokana na kashfa hiyo ambayo imelipaka tope shirikisho lakini pia mpira wa miguu kwa ujumla.

Clip hiyo ya sauti inayosemekana ni ya baadhi ya maofisa na viongozi wa juu wa TFF imeanza kusambaa tangu juzi jioni na kuzua mijadala mbalimbali kwa wadau wakihoji juu ya hatma ya soka la nchi hii kwa staili ama mtindo huu wa mwenye pesa ndiye anafanikiwa katika soka la bongo.

Na tangu kuenea clip hiyo tayari aliyekuwa mkurugenzi wa mashindano wa TFF Martin Chacha ambaye naye inasemiekana amesikika katika clip hiyo aliamua kubwaga manyanga katika nafasi hiyo huku taarifa ya kuondoka kwake TFF waliitoa kwamba kiongozi hiyo wa kamati ya mashindano ambaye alikuwa pia mratibu wa timu zote za taifa amejiondoa kutokana na kubanwa na majukumu ya kikazi hivyo asingekuwa na muda wa kutosha kuutumikia mpira na TFF ikamtakia kila la kheri huko aendako.

Hali hiyo imeendelea kuchukuwa sura mpya mara baada ya hapo jana Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine kumsimamisha aliyekuwa mshauri wa masuala ya ufundi wa rais wa TFF Juma Matandikaili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazohusiana na hadhi za wachezaji (players status).

Taarifa ya TFF imesema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa ibara ya 266,267 na 268 ya Kanuni za Utumishi za TFF toleo la mwaka 2015.

Pamoja na hatua hizo za baadhi ya viongozi kujiuzuru ama kusimamishwa lakini wadau wa soka wameona adhabu zilizotolewa na kamati ya nidhamu ya TFF kwa wachache waliokutwa na hatia ni wazi wameonewa ama kubebeshwa mzigo usio wahusu hivyo wamesisitiza kuwa wahusika wakuu wa sakata hilo la rushwa na upangaji matokeo washughulikiwe kwa mujibu wa sheria na adhabu kali zitolewe kwa watakaobainika kufanya mchezo huo mchafu.

Aidha Wadau hao wakaenda mbali zaidi kwa kumtaka rais wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF Jamal Nalinzi kubwaga manyanga ama kujiuzuru wadhifa wake wa urais kwakuwa hata kama yeye hajahusika kama anavyosikika akijitetea katika vyombo vya habari lakini clip ya sauti zinazosemekana ni za maofisa na viongozi wa juu wa shirikisho analoliongoza basi ni wazi hawezi kukwepa kufanya uamuzi huo kwa maslai ya mpira na pia kutunza heshima yake.

Wadau hao wa soka wamesema kwa kashfa hiyo Malinzi na taasisi hiyo kubwa kabisa ya michezo nchini wameingia doa na ni dosali kubwa katika mpira nchini hivyo ni wazi wanapaswa kuwajibika si Malinzi bali na hata kamati zake zote hasa secretarieti zake kwa ujumla.

Wakimalizia wadau hao wamesema kuna wadau wamejipanga kufanya maandamano ya amani kuutaka uongozi mzima wa TFF chini ya rais wake Jamal Malinzi ujiuzuru kama hautafanya hivyo ndani ya siku saba kuanzia sasa kwa maslai ya mpira.

Wadau hao wamesema Malinzi na kamati zake wasione haya kuchukuwa uamuzi huo kwani sio wa kwanza kufanya hayo ikumbukwe hata viongozi wa juu wa FIFA walichukuwa uamuzi huo ili kupisha uchunguzi kwani kujiuzuru sio hakutokufanya wewe uonekane ndiye muhusika walimaliza hivyo.