Jumanne , 25th Nov , 2014

Shirikisho la soka nchini TFF,limewataka wananchi mbalimbali kuanza kupiga kura ikiwa ni sehemu ya kuchagua jezi mpya ya timu ya taifa,Taifa Stars.

Akizungumza na East Africa Radio,Mkurugenzi wa Michezo wa TFF,Boniface Wambura amesema kura hizo zitapigwa kupitia mtandao wa TFF ambapo jezi hizo zimeweka huku mwisho wa kupiga kura ikiwa ni Desemba 31.

Wambura amesema wamepokea mapendekezo ya jezi hizo kutoka kwa watanzania 86 ambapo ni Jezi 11 za nyumbani na Bukjta nane za nyumbani huku jezi nane zikiwa za ugenini na Buj\kta tano za ugenini.